MAJIBU 10 YANAYOULIZWA NA MARAFIKI WANGU MARA KWA MARA!!!
1. R.O.M.A ni muumini wa dini ya kikristo(R.C) aliyezisoma
sakramenti zote 7 na kupokea ya ubatizo/ekaristi takatifu na hata
kipaimara...nangoja NDOA!!
2. Ile sauti mnayosikiaga ikisema
TONGWE RECORDS BEIB siyo ya ROMA ni JOSLIN!!ambae naye ni
miongoni mwa wasanii walio chini ya tongwe!! plus KAMIKAZE/JOS
MTAMBO/DOMO KAYA/SAIGON/NORMAN WA BSS/
3. Kuna J. MURDER ambae ndiye CEO wa tongwe records, na kuna
J.RYDER ambaye ndiye anagonga midundo ya TONGWE RECORDS. watu
wawili tofauti!!
4. Tongwe records ni studio zilizopo
daresalaam mitaa ya masaki/ dakika kama 3 tu kutokea coco beach!! na
haipo kigamboni kama wengi wanavyodhani!! lakini tanga kuna kijiji
kinaitwa TONGWE na ndicho kijiji ama himaya ya J. MURDER!! ambaye
ndiye huyo mmiliki!!
5. Sijawahi kufungwa wala kwenda jela/
sijawahi kuitwa ikulu/ nyimbo zangu za awali tanzania/ mr president
ndiyo zilipigwa stop kupigwa ktk baadhi ya vituo vya radio, kwa sababu
zao binafsi!!
6. Mimi kwetu ni TANGA nimezaliwa na kukulia
na kusoma na kuanza muziki TANGA/ kiasili ni mpare(SAME KILIMANJARO) na
mama ni mchaga!! kikabila utani unaruhusiwa, mpare mtani wake mchaga,
ndiyo maana mchaga siku zote namuona ni mtani wangu(MSIPANIKI)!!
nadumisha mila ya utani!!
7. Katika face book account yangu
niitumiayo ni hii ya Roma Tongwe na pia kuna page yangu inaitwa
R.O.M.A na kuna group inaitwa ONGEA NA ROMA baaaasiii!! lakini kuna
wana tu kwa mapenzi yao ama kwa uduanzi wao huamua na wamefungua akaunti
kibao wakijiita Roma mkatoliki/Roma mtanzania/Roma Tanga/ na zingine,
tena ukizipitia jamaa wana marafiki wengi kuliko hata mimi, na
wanazi-run kama mimi yaani nao wanapost kabisa ETI OYAA MOROGORO HERE I
COME...hahahahahha bongo bana!!
8. Aliyeimba chorus ya 2030
ni mtoto wa rafiki yangu anaitwa STORY, ni mtoto wa miaka 7hiviii!!
lakini chorus ile iliimbwa miaka ya 90 naa zamani sana na binti mmoja
ambaye kwa sasa amekuwa sana!!!
9. Nilianzisha mtindo wakuuza
nyimbo zangu on-line(BUT LOKO) na kama trial nilianza na 2030(tsh
3000/=), ilikuwa ni nyimbo inayohitajika sana na wenye mapenzi na kuujua
umuhimu wa kazi ya sanaa walinunua(sio woote) ila kati ya marafiki 5000
wa fb walinunua takribani watu 500 tu!! hadi sasa siwezi na sijawahi
mtumia mtu nyimbo yangu akiniomba for free!! it z for sale!! 3000 per
track!! otherws tumia indirect ways!!
10. Natoa ngoma 1 kwa
mwaka!! tokea naanza game hii, ndiyo utaratibu niliojiwekea, najaribu
kufanya LIVING SONGS!!(nyimbo zinazodumu/zinazoishi, kana kwamba
ukisikia jogoo la tanzania linawika sasa uamke kwenye kiti chako turuke
ruke!!) wapo artist ambao ndani ya miezi 6 wanatoa ngoma hata 4, na
zinaweza feli zote, ama zikafaulu zote!! ni sawa kwa upande wao!!ndio
njia waliyoichagua!! So toka tanzania 2008 hadi 2030 iliyotoka
december 29 2012 siku moja kabla ya 2013!! ipo hivo!!
kwahiyo nadaiwa ngoma mpya mwaka huu!! na SOON ZITATOKA VIDEO 2 ZA ROMA!!
SIJARUHUSU NIULIZWE SWALI JINGINE!!!
tutajibu mengine siku nyingine!!
love love marafiki wake mimi apa!!
Rooomaaa!!!A
© Dvj Sweetp Dj | Radio Producer | Sales and Marketing | Social Media Admin
For hire +255 753 672 877
0 comments:
Post a Comment