Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga
pichani kulia, mara baada ya kumaliza ziara ndani ya kampuni hiyo na
kujionea mambo mbalimbali, Kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Tigo Alice
Maro.
Meneja
Mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo akifanya mahojiano mafupi na
Mtangazaji wa Choice FM, Thandi Kathembe mapema leo jioni.
Mkuu wa
Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga (pili kutoka kulia), akifafanua
jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego
Gutierrez alieambatana na Ofisa Mahusiano wake, Alice Maro, kulia ni Dj
Fetty.
Mkuu wa
Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu
wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez (pichani
kati),Kulia ni mmoja wa watangazaji wa Clouds FM, Ruben Ndege.
Meneja
Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez akiperuzi
moja ya jarida la Burudani hapa nchini la KITANGOMA, linalochapishwa na
kampuni ya Prime Time Promotions LTD.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga akimuelekeza
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego Gutierrez
namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikiwa tayari kwa kurushwa
hewani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga
akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo, Diego
Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikitayarishwa kabla
ya kwenda kurushwa hewani.
Picha na The Habari







0 comments:
Post a Comment