Blogger Widgets
Home » » Tamasha | TAMASHA LA UTEUZI TUZO ZA GRAMMY DISEMBA 05

Tamasha | TAMASHA LA UTEUZI TUZO ZA GRAMMY DISEMBA 05


Picha ikionesha namana jukwaa litakavyokuwa.

Uteuzi wa Tamasha la Grammy utafanyika Disemba 05 ya Mwaka huu 2012 katika Mji wa Nashville Tenn katika Uwanja wa Brigdestone nje kidoga ya Mji wa Los Angeles hii ikiwa ni mara ya kwanza na pekee kwa tuzo tamasha la tuzo hizi kufanyika nje ya Los Angeles.


Rais wa Tuzo hizi Neil Portnow ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo cha Kurekodi Muziki Nashville, amesema Muziki ni tamaduni isiyofutika na ni utajiri mkubwa hivyo wamedhamilia kuuadhimisha Mwaka kitofauti na tuzo hizi  Grammy, pia jumla ya Tuzo 55 zitatambulishwa kwa ajili ya kushindaniwa.

Tuzo hizi zimeweza kuvutia jumla ya watazamaji Milioni 39.9 tangu mwaka 1984. Ticketi, Watangazaji na Wasanii watakaoshiriki  tamasha la Uteuzi la Tuzo za Grammy itatangazwa katika wiki inayokuja.


© Sweetbert Philemon This Is HABARI™

0 comments:

Post a Comment

.