
Kaka ameitwa kuichezea Brazil kwa ajili ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki dhidi ya Iraq na Japan Mwezi ujao baada ya kutochukuliwa tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa huko Afrika Kusini.
Tangu atue Real Madrid, Kaka, Miaka 30, amekuwa na wakati mgumu lakini hivi karibuni nyota yake imeanza kung’ara tena na Jumatano aliifungia Real hetitriki walipocheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Colombia Millonarios.
Kocha wa Brazil, Mano Menezes, ameamua kumchukua Kaka ili kumpima uwezo wake katika Mechi hizo mbili ambazo zote zitachezwa Ulaya.
Mechi ya Brazil na Iraq itachezwa huko Malmo, Sweden hapo Oktoba 11 na ile ya Japan itachezwa Wroclaw, Poland hapo Oktoba 16.
Kikosi hicho cha Brazil kina Wachezaji wanne ambao wanachezea Klabu za Ligi Kuu England ambao ni watatu kutoka Chelsea, David Luiz, Oscar na Ramires, na Kiungo wa Tottenham Sandro.
Kikosi kamili:
Makipa: Diego Alves (Valencia ), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico-MG)
Mabeki: Daniel Alves (Barcelona ), Marcelo (Real Madrid), Adriano (Barcelona), Alex Sandro (Porto), Thiago Silva (PSG), David Luiz (Chelsea), Dede (Vasco), Leandro Castan (Roma)
Viungo: Sandro (Tottenham), Paulinho (Corinthians), Fernando (Gremio), Giuliano (Dnipro), Lucas Moura (Sao Paulo), Oscar (Chelsea), Ramires (Chelsea), Thiago Neves (Fluminense), Kaka (Real Madrid)
Mastraika: Neymar (Santos), Leandro Damiao (Internacional), Hulk (Zenit)
© Sweetbert Philemon This Is HABARI™
0 comments:
Post a Comment