Blogger Widgets
Home » » Michezo | Man City, Everton West Ham kutolewa CAPITAL ONE CUP

Michezo | Man City, Everton West Ham kutolewa CAPITAL ONE CUP



CAPITAL_ONE_CUP-BEST

















Mabingwa wa Soka England, Man City, jana wakiwa kwao Uwanja wa Etihad wametupwa nje ya CAPITAL ONE CUP, ambalo kabla lilikuwa likiitwa Carling Cup, baada ya kufungwa Bao 4-2 na Aston Villa katika Mechi ya Raundi ya 3 iliyochezwa Dakika 120 baada ya kutoka sare 2-2 katika Dakika 90.
Katika Mechi nyingine za Raundi hiyo, Everton ilifungwa 2-1 na Leeds United na kutolewa huku West Ham wakichapwa 4-1 na Wigan na kutupwa nje.
Mechi za Raundi ya 3 zinaendelea tena leo Usiku huku Mabingwa watetezi wakicheza ugenini na West Bromwich Albion.

MATOKEO=RAUNDI ya TATU:
Jumanne Septemba 25
Bradford 3 Burton 2 [Baada Dakika 120]
Chelsea 6 Wolves 0
Crawley 2 Swansea 3
Leeds 2 Everton 1
Man City 2 Aston Villa 4 [Baada Dakika 120]
MK Dons 0 Sunderland 2
Preston 1 Middlesbrough 3
Southampton 2 Sheff Wed 0
Swindon 3 Burnley 1
West Ham 1 Wigan 4

RATIBA=RAUNDI ya TATU:
Jumatano Septemba 26
[Mechi kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Man United v Newcastle
QPR v Reading
Norwich v Doncaster
Arsenal v Coventry
Carlisle v Tottenham
[Saa 4 Usiku]
West Brom v Liverpool

© Sweetbert Philemon This Is HABARI™

0 comments:

Post a Comment

.