Blogger Widgets
Home » » MUZIKI | SUMA MNAZARETI KUJA "TUKO WANGAPI?" MAPEMA HII

MUZIKI | SUMA MNAZARETI KUJA "TUKO WANGAPI?" MAPEMA HII



Huku akihit sana na Chuku time Msanii Suma Mnazareti amesema anajiandaa kuja na wimbo wake mpya uitwao "Tuko wangapi" wimbo ambao amemshirikisha Tundamani.
Suma amesema wimbo wake huo unazungumzia hasa wanawake ambao wamekuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja, jambo ambalo sio zuri hata kidogo. Hivyo ameamua kuuliza tuko wangapi?
Wimbo huu pia ukiwa ni fundisho kwa wanaume ambao wanatamaa na wanawake, wakimtaka kila mwanamke bila ya kujua ni nani yuko na Mwanamke huyo.

"Hii itakuwa kazi ya taifa kwani nimejipanga kufunika bongo nimekuja kwenye kuwakimbiza si kama demu wa bongo movie alivyodhani nimekuja kupoteza muda najua mzigo utakuwa sokoni lazima wake kimya" Alisema wakati akizungumza na mtandao wa Dartalk

Tangu Suma Mnazareti kuachia wimbo wake wa Chukua Time mwaka jana , umekuwa ni wimbo ambao unashika nafasi za juu, katika chati mbalimbali za muziki.
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™

0 comments:

Post a Comment

.