Blogger Widgets
Home » , , , » MUZIKI | ONE LOVE FX;STUDIO YENYE STADI NA UWEZO WA KIMATAIFA KATIKA KUANDAA MUZIKI.

MUZIKI | ONE LOVE FX;STUDIO YENYE STADI NA UWEZO WA KIMATAIFA KATIKA KUANDAA MUZIKI.


Kama ni Production ya Muziki kwa sasa nchini Tanzania One Love Fx Studio, kupitia kwa Producer wake Mkali Tiddy Hotter imeweza kudhihilisha uwezo wake mkubwa wa kuleta mapinduzi mapya katika uzalishaji wa Muziki huu. Umahili huo umeonekana katika nyimbo ambazo zinafanya vizuri katika Muziki ikiwa ni nyimbo ya Belle 9 - Listen up pamoja na Track ya Mwanachemba DarkMaster, lakini pia kukiwa na nyimbo nyingine nyingi. Hii ni moja ya Interview ambayo tumeifanya na Producer Tiddy Hotter kuhusiana na One Love Fx, kubwa likiwa ni kufanya Muziki katika Level ya Kinataifa.

INTERVIEW NA ONE LOVE FX – Prod. Tiddy Hotter.



Swali : One Love Fx. Labda kwa ufupi ina Muda tangu imeanza kazi na inapatikana wapi?

Tiddy. One Love Fx Kwa sasa ina muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu, one love fx inapatikana Ilemela Mwanza..

Swali : Ni nani Mhusika Mkuu wa One Love Fx?
Tiddy. Nashkuru kwa swali hili, kwa ufupi One Love Fx ni “muungano” hivyo basi kuna mhusika mkuu kwa kila kitengo, huku mimi nikiwa ni mkuu wa kitengo cha Audio Production.

Swali : One Love Fx inshughulika na Mziki wa Audio pekee au imegawanyika katika kazi mbalimbali?

Tiddy. Hapana One Love Fx haishughuliki Audio tu bali inashughulika na videos na filamu, huku videos na filamu zikifanywa na Hypa Ibadah na pia director wa filamu akiwa Shaibu Kassim






Kutoka Kushoto ni Shaibu,Tiddy Hotter na Hypa Ibadah


Swali : Jiji la Mwanza limekuwa nyuma katika Production ya Muziki, Je, ni mkakati upi uliopo kuirudisha Mwanza katika hadhi yake ya Kimuziki?

Tiddy. Kwanza ni kufanya kazi bora yaani zenye viwango vya kimataifa la pili ni kuwaelemisha wasanii ili waelewe kwamba kitu wanachokifanya ni biashara kubwa sana duniani na la mwisho ni kuhakikisha tunatumia vilivyo mazingira yetu ya Mwanza katika kufanya mambo mbalimbali ya kisanaa!

Swali : Je, ni vigezo vipi ama Masharti gain yatakayomwezesha msanii kuweza kurecord katika Studio ya One Love fx?

Tiddy.One Love Fx humsaidia msanii yeyote Yule hata kama akiwa tayari amekua nyota, na vile vile hutoa aina flani ya msaada kwa wasanii wasiojiweza kifedha kwa mkataba maalum ulithibitishwa kisheria, pia hili hufanyika kwa msaanii mwenye vigezo vya hali ya juu sana ili aweze kurudisha mkopo wake.

Swali : One love Fx inafanya kazi kama label ili kumiliki kazi za wasanii mbalimbali au ni msanii anarecord na kuondoka?
Tiddy. Hapana One Love Fx haifanyi kazi kama label, bali itaendelea kuwa mmiliki wa kazi siku zote, kupitia makubaliano ya umiliki.

Swali : Mpaka sasa kuna kazi kama Listen ya Belle 9 na Tusomane ya Dark master na zinafanya vizuri, Je, kuna kazi nyingine ambazo zitaachiwa hivi karibuni?
Tiddy. Asante kwa swali zuri, jibu ni NDIYO! Kuna mfululizo wa kazi nyingi zinakuja mwaka huu zikiwemo za wasanii kutoka nje ya nchi na bara hili la afrika

Swali : Changamoto gain ambazo umekuwa ukizipata kama Producer kutoka kwa Wasanii wanofika kwa ajili ya Kurecord?
Tiddy. Changamoto kubwa ni tatizo walilonalo wasanii wadogo : nalo ni kuiga miziki inayohit kwa wakati huo hivyo kuongeza wingi wa kazi zinazofana ladha, ni hilo tu mengine huwa tunarekebishana taratibu.


Producer Tiddy Hotter wa One Love Fx

Swali : Studio mbalimbali zimekuwa zikitengeneza project mbalimbali ikiwemo kutengeneza albamu na kuwainua baadhi ya wasanii, kitu ambacho mara nyingi kimekuwa kikifell, Je, kwa upande wa One love Fx kuna project zozote ambazo zimeandaliwa?
Tiddy. Kiukweli One Love Fx inajipanga kufanya kazi kubwa kama hizo ili zisifeli kama hizo uzisemazo kwa sababu sio kazi za kukurupuka tu! Ukazifanya

Swali : Mchango mkubwa wa Media na watu mbalimbali husaidia kwa Studio kukua na kutambulika zaidi, Kwa One Love Fx Mchango huu unapatikana?

Tiddy. Kwa nafasi hii nasema “ndiyo” japokua sio saana kama wenzetu wengine ambao ni dhahiri tumewazidi ufundi.

Swali : Nini msisitizo wako kwa Wasanii hususani wa Kanda ya Ziwa na mahali pengine?
Tiddy. waache kuigaiga ovyo coz wanao uwezo wa kufanya ya kwao na vile vile waepuke suala la kukwepa budget za mziki hasa kurekodi rekodi kwa bei ndogo kwenye studio zisizo na viwango

© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™

.