Blogger Widgets
Home » » MUJUE AMINA CHIFUPA IKIWA NI MIAKA MITANO TANGU ATUTOKE

MUJUE AMINA CHIFUPA IKIWA NI MIAKA MITANO TANGU ATUTOKE


Amina Chifupa enzi za uhai wake


vichwa vya habari katika magazeti siku ya 26 Juni 2007 ilikuwa ni habari ya kufariki kwake.
siku Amina Chifupa akiapa bungeni enzi za uhai wake
 
Video ambayo inahusu mazishi yake(Amina Chifupa)

HISTORIA FUPI YA AMINA CHIFUPA

Amina Chifupa Mpakanjia alizaliwa tarehe 20 Mei, mwaka 1981 na amefariki tarehe 26 Juni, 2007. Mh. Chifupa alisoma shule ya msingi Ushindi na kujiunga na masomo ya sekondari Kisutu kabla ya kuingia shule nyingine ya sekondari ya Makongo alikomaliza elimu ya kidato cha sita mwaka wa 2001.
Mh. Amina Chifupa alikuwa Mbunge wa kiti maalum kupitia tiketi ya Vijana na alikuwa kiongozi anayepiga vita dhidi ya utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Kabla ya kumaliza masomo yake Mh. Amina alikua mtangazaji wa redio iitwayo clous FM, katika kipindi akiwa mtangazaji aliweza kuvuma sana kutokana na sauti yake iliyokua nyororo na ya kuvutia haswa kwa vijana wenzake. Aliendelea na kazi hii ya utangazaji pale alipomaliza masomo yake hadi alipoteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu katika serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya nne.
Na sasa ni miaka Mitano tangu atutoke.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA CHIFUPA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

0 comments:

Post a Comment

.