
Jack Wolper nyota wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya
filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper amefunguka kwa kusema kuwa kuna
mtangazaji mmoja ambaye amekuwa akitumia nafasi yake kwa kumpiga vita na
kumzushia kashifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujaribu kumtengenezea
mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike, Jack
amesema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa gari yake aina BMw X 6 kuwa
amenyeang,anywa.

Jack Wolper akiwaonyesha kadi ya gari Bmw x6 waandishi wa habari hawapo pichani.

Bmw x 6 aina ya gari kama la Jack Wolper.
“Kuna mwanadada ambaye amekuwa
akieneza habari za uzushi kuhusu mimi ikiwa na kuhakikisha kuwa mimi
ninakosana na wasanii wezangu, kama hivi karibuni nikiwa location rafiki
zangu walinipigia simu wakinijulisha kuwa kuna habari zinatangazwa
katika Redio pamoja na baadhi ya mitandao zikisema kuwa mimi
nimenyang,anywa gari langu la Bmw habari ambazo si kweli gari langu lipo
ndani nyumbani kwangu,”anaongea Jack kwa uchungu.
Mwanadada huyo amesema kuwa yeye ana
gari zaidi ya moja kwa hiyo hakuna mtu wa kumpangia atembelee gari gani
kwani katika taarifa hizo ilisemekana kuwa kuwa alikuwa kitembelea gari
aina ya Noah gari yake ya awali, akiongea zaidi alisema kuwa habari za
kumchafua zimekuwa zikitengenezwa na mwanadada mmoja ambaye ni
mtangazaji lakini akasema kuwa hana sababu ya kumtaja kwani anajijua.Kwa
habari hii na nyinginezo zinazohusu tasnia ya filamu Bofya Hapa
source:http://viwanjani.blogspot.com
source:http://viwanjani.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment