Kutokana na hali inayoendelea kujitokeza kwa sasa nchini, machafuko mbalimbali ya kisisa na kidini yamekuwa yakitishia uwepo wa Amani Tanzania kama ilivyozoeleka mwanzo, hadi kufikia baadhi ya wananchi kuona si vema kuwapo tena katika nchi hii, kwa kuhofia machafuko makubwa kujitokeza. Kwa yote hayo Mtunzi wa Mashairi Bwana ELIBARIKI MADIHI hayuko mbali katika kuliongelea hili suala kupitia ushairi wake, na haya ndiyo mawaidha yake.
Hebu tuelewane hapa
Nauliza wadendwa hivi nani mwenye haki
anayefaa kupendwa sita sema mnafiki
vyombo vilivyo undwa
vinavyo tetea haki
au mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni
Maskini wanateseka haki hazionekani
wamebaki wanabweka wamejifungia ndani
wale wenyemadaraka wamewaziba midomoni
ndo tunavyojifariji kuwa hinchi hii ya amani
Amanigamba la nje lakini ndani hakuna
kwasifa nchi zanje vitambi wana vikuna
gusamadeni ya nje wanajifanya wanaguna
kwanini walio wengi hawaachii madaraka
Wimbi laumasikini bodo linaongezeka
raia wenye amani ipo siku watachoka
uchafu madarakani halafu wanauzika
hivi we unaamini bado kuna shule za mamiti
Hata mtoto mdogo humdanganyi kwa pipi
wakushindia mihogo ukamwambia mambo vivpi
Tanzania sio ndogo tunaachiwa makapi
acheni watajirike tunabaki na mashimo
Jamani kuna baadhi yamambo yanakela sana najua watu na
wananchi wana mengi yaku sema ila wanashindwa watayasemea wapi na wanao pata
nafasi yakutetea wanyonge wanasakamwa kama mamwawe yanavyo sakama kuku lakini
wananchi ipo siku watachoka tu big up kwenubwa na Faraja Mwepea (
CHIBA WA NGOMBELEZO KULIKO WACHILUMANGA)
© Sweetbert Philemon This Is HABARI™
0 comments:
Post a Comment