Zikiwa ndio Tarehe za mwisho katika kuumalizia huu Mwaka 2012. Katika Anga la Michezo Ligi mbalimbali zilikuwa zikiendelea pande zote Duniani, na hasa hapa kwetu Nyumbani Tanzania.
Vilabu mbalimbali vilichuana katika Mechi ambazo zilikuwa katika Ratiba na Mashabiki wa Mpira wa Miguu kuburudika kwa shangwe nyingi, pale tu Timu zao zinapofanya vizuri.
Kwa Mujibu wa Mtandao mmojawapo wa Kimichezo Duniani, hii ndiyo Idadi ya Mabao ambayo yamefungwa katika Ligi kuu Tano 5 Ulimwenguni ambazo zinafanya vizuri katika Kandanada.
1. ENGLISH PREMIER LEAGUE - EPL
Ikiwa ndio Ligi inayoongoza kwa Umaarufu mkubwa Duniani ina Jumla ya Mabao 501
2. SERIA A
Nafasi ya pili ikiwa kwao, Ligi hii imekuwa na Jumla ya Mabao 496
3. LA LIGA
Katika Nafasi ya Tatu ina jumla ya Mabao 485
4. LIGUE 1
Katika Nafasi ya 4 imefikisha jumla ya Mabao 459
5. BUNDESLIGA
Katika nafasi ya Tano ina jumla ya Mabao 444
Hivyo kufanya Jumla ya Mabao 2385 Katika Ligi hizi kubwa Ulimwenguni na Maarufu.
© Sweetbert Philemon This Is HABARI™
0 comments:
Post a Comment