Mwanamuziki Kala Jeremiaha, amethibitisha rasmi kuwa Wimbo wake ambao aliutoa Mwanza jana na unaopatikana katika, Album ya PASAKA, "Dear God" ni wimbo ambao umefanya na unaendelea kufanya vizuri katika pande zote za Afika Mashariki hasa katika nchi za Kenya, Burundi na Tanzania.
Kutokanan na maelezo ya Kala Jeremiah, amesema wimbo huo umekuwa ni wimbo wa kwanza wa Hip Hop, ambao umekubarika katika rika na aina mbalimbali za watu.
"DEAR GOD INAZIDI KUFANYA VIZURI SANA AFRICA
MASHARIKI,HASA KENYA BURUINDI NA TANZANIA,LAKINI PIA UTAFITI UNAONYESHA
KUWA DEAR GOD NI WIMBO WA KWANZA WA HIP HOP KUTOKEA BONGO KUKUBALIKA KWA
WATU WA AINA NA LIKA ZOTE, HAPA NAMANISHA, MAASKOFU, WACHUNGAJI MA
PADRI,MAIMAMU, MASHEKHE,WALOKOLE, WAISLAM,WAZINZI, VIBAKA, WABABA,
WAMAMA, WATOTO,MASELA, NA MASISTER DU.KWA KIFUPI KILA MTU ALIYEUSIKIA
KAUKUBALI KWA ASILIMIA MIA" amesema Kala Jeremiah.
Wimbo wa Dear God ni wimbo ambo umetuma ujumbe kwa kila Mtanzania, Hivyo Msanii Kala Jeremiah anazidi kushukuru kwa kazi ambayo ameifanya katika wimbo huo.
"hili kwangu ni
bonge la zawadi,ASANTE MUNGU,lakini pia umekuwa wimbo wa kwanza
kutengeneza MESEJI (sms) AMBAYO IMETUMWA KARIBU KWA KILA MTANZANIA
MWENYE SIMU.ASANTE MUNGU,lakini pia umekuwa kati ya nyimbo chache sana
za hip hop TANZANIA ambazo hata dada zetu wameweza kuzikariri na
kuuchana.HIYO INAONYESHA KUWA HIP HOP INAPENDWA NA KILA MTU. ASANTE DEAR
GOD KWA HILI SHAVU JINGINE."amesema Kala Jeremiah.
Kala Jeremiah ni Msanii ambaye alianza kutamburika katika tasnia ya Muziki tangu kipindi cha shindano la Bongo Star search 2010, akiwa na wimbo wake wa Mama alisema akiwa amemshirikisha Makamua, pia katika wimbo ambao alifanya na Naakaya Msanii kutoka Arusha "Wimbo wa Taifa. Nyimbo nyingine nyingi ambazo amefanya yeye mwenyewe pamoja na wasanii wengine kama Roma, Bella Kombo na Jokate.n.k
Kwa sasa Albamu ya Kara Jeremiah iitwayo Pasaka inapatikana mtaani kwa kiasi cha Shilingi 5000/= tu huku ikiwa na idadi ya nyimbo 22, ambazo Kala Jeremiah amezifanya.
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link
0 comments:
Post a Comment