Blogger Widgets
Home » » MUZIKI | LADY JAY DEE NA PROFESSOR JAY PAMOJA TENA WAKIWA NA "JOTO,HASIRA"

MUZIKI | LADY JAY DEE NA PROFESSOR JAY PAMOJA TENA WAKIWA NA "JOTO,HASIRA"


 Nguli wawili wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini Tanzania, Nawazungumzia Lady Jay Dee(Binti Machozi) na The Heavy Weight Mc Professor Jay, sasa wanarudi tena katika Ulimwengu wa Muziki na Kibao cha "JOTO, HASIRA" kitakachota hivi karibuni!

Huku tukirejea katika kumbukumbu wakali hawa wameshawahi kufanya Collabo ya Muziki na ika hit vilivyo katika Nyimbo wa Professor Jay "Bongo Dar es Salaam na Nimeamini" Nyimbo ambazo zilifanya vizuri sana, na hadi sasa ni nyimbo ambazo ni hazina katika Muziki wa Bongo Fleva.
Hii ni nguvu nyingine ya pamoja tena katika Muziki huu, kutokana na Sauti hizi hatujazisikia zikiwa pamoja kwa muda mrefu hivi sasa.

Kupitia Mtandao wa Kijamii Facebook, Binti Machozi ama Lady Jay Dee aliandika ujumbe huku akijumuisha picha nne za CD cover ya wimbo huo.

"Naomba ku share muonekano wa ndani wa CD ya wimbo wangu mpya “JOTO, HASIRA” feat Prof Jay ambao unatoka siku za karibuni.” Lady Jaydee aliwaomba mashabiki wake wamsaidie kuchagua kava la wimbo huo"
 Tunasubiri kusikiliza hit flavour ya wakali hawa!
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™

.