Blogger Widgets
Home » , , » NOKIA 105 | INAYOKAA NA CHAJI SIKU 35, ITAUZWA Tsh. 30,00/=

NOKIA 105 | INAYOKAA NA CHAJI SIKU 35, ITAUZWA Tsh. 30,00/=Baada ya Nokia 1100 huenda Nokia 105 ikaja kuwa simu maarufu zaidi hasa kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Hii ni baada ya kampuni hiyo ya simu kuzindua simu hiyo yenye uwezo wa kutunza chaji kwa siku 35 kila unapochaji.

Simu hiyo imetengenezwa maalum katika maeneo ambayo umeme hakuna ama unasumbua lakini pia kama ‘backup phone’ pale zingine zinapozima.

Ikiwa inatarajia kuingia sokoni wiki kadhaa zijazo, Nokia 105 ambayo bei yake ni paundi 13, sawa na shilingi 30,000 za Tanzania pia ina tochi na FM radio.
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™