Mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Fichuka Development Agency LTD, Frank Fichuka amesema ili kuhakikisha DVD ya Nikki wa Pili, Bum Kubum inawafikia wananchi wengi, imepanga kufanya promotion ya mwezi mzima. Pamoja na hivyo Nikki wa Pili amepanga kutoa zawadi kwa mashabiki waliomuunga mkono kwa kununua DVD hiyo.
“Ndani ya mwezi mmoja tunajaribu kufanya kama promotion fulani hivi ambayo mtu kwenye mtandao wowote anaweza kununua,” Frank amesema. “Mtandao wowote mtu unaweza ukanunua. Tunajaribu kuangalia njia convenient kwake halafu vilevile kwa wakazi wa Dar es Salaam tutakuwa tukifanya free delivery. Watu watakuwa wanaplace order jinsi ya kuplace order ni rahisi tu. Kwa wakazi wa Dar es Salaam unaandika tu mahali ulipo unatuma kwenye namba yetu ambayo ni 0655 671 550.”
Frank amesema baada ya hapo watampelekea mteja DVD yake mpaka mahali anapoishi na kudai kuwa wameingia makubaliano na waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam kwa kazi hiyo. Ameongeza kuwa Nikki wa Pili amepanga kutoa zawadi kwa mashabiki waliomuunga mkono kununua DVD hiyo.
“Mpaka sasa hivi hajasema ni zawadi gani atatoa lakini bado yupo kwenye mchakato very soon atatangaza.”
Ameeleza kuwa mwezi uliopita, wameuza kopi 703 ya DVD hiyo yenye gharama ya shilingi 4,000. “Sisi kama sisi tunaona ni mafanikio makubwa kuweza kuuza nakala hizo kwanza ni kitu kipya kabisa, halafu tulikuwa tunafanyia mtandao mmoja kwamba walikuwa ni wateja tu wa M-Pesa halafu ilikuwa ni mikoa mitatu, Dar es Salaaam, Arusha na Kilimanjaro. Hiyo ilikuwa ni changamoto kwa watu wa mitandao mingine.”
0 comments:
Post a Comment