Blogger Widgets
Home » , » STORY | Je Unajua Beyonce alishawahi kusalitiwa mara ngapi na Mpenzi wake??

STORY | Je Unajua Beyonce alishawahi kusalitiwa mara ngapi na Mpenzi wake??


 Mapenzi yamekuwa na mtizamo wa kila aina , pamoja na uzuri wote huu, lakini usaliti ulitokea tu kwa Mwanadada Beyonce. Stori nzima ni hivi :-

Lyndall Locke ambaye alikuwa mpenzi wa Beyonce kuanzia Mwaka 1993 hadi 1997, amekubali kuwa alimsaliti mara Tano Mwanadada Beyonce wakati wakiwa wapenzi.

Akizungumza na Gazeti la "The Sun"  la U. K , Locke amesema yeye na Beyonce walikuwa wapenzi wa Ujanani, lakini hakuwa kuwa mwaminifu kwa Mwanadada huyo kitu ambacho kinamuumiza zaidi mpaka sasa. 
Locke akiwa na Beyonce

Amesema uhusiano wao ulianza kupungua na hatimaye kufikia mwisho kabisa, pale Beyonce alipoanza kutambulika na kuwa maarufu wakati akiwa katika kundi la Destiny Child. Kadri Beyonce alivyozidi kuwa star na mtu maarufu zaidi, mwanaume alijiona kuwa sasa si mtu wa kuweza kuwa na Beyonce tena.

Aliongeza zaidi kuwa siku moja Beyonce alipokuwa ametoka, mwanaume huyo alienda bar na rafiki zake na kulala na mwanamke mwingine. "Nilimcheat Beyonce mara tano lakini hakujua na sikumwambia mpaka pale tulipo achana" alisema Locke
Mapenzi enzi hizo locke na beyonce

Locke alijitahidi kutumia nafasi nyingine kurudiana na Beyonce lakini ikawa ngumu zaidi pale Beyonce alipoanza mahusiano na Jay Z
Beyonce na Jayz

Nani anaweza kumcheat mwanamke mzuri kama Beyonce? Ni mimi locke alisema, huku akiumia zaidi kwani ni mwanamke ambaye hawezi kumpata tena tangu amekuwa katika mahusiano na Jayz, lakini alimaliza kwa kusema, hakuna namna ya kurudiana na Beyonce lakini ataendelea kunipenda tu.

Katika Interview ambayo Beyonce aliifanya 2008 na "The Telegraph" alisema alishawahi kuwa na mwanume mwingine kabla ya kuwa na Jayz


© Dvj Sweetp Dj | Radio Producer | Sales and Marketing | Social Media Admin For hire +255 753 672 877

0 comments:

Post a Comment