Msanii
wa kwanza kufanya album hapa Bongo na kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini
kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II na wengi
hupenda kumuita Sugu ameonyesha wazi kukerwa na ambao ameuimba ROMA
katika ngoma yake ya 2030, Sugu alichodai ROMA ana kurupuka na hajui
anachokifanya.
Sugu amesema kuwa msanii huyo
anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu amemuonya na kumtaka
roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa kwa jamii na sio
kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini.
Sugu
amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip hop
lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na si
kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe
muangalifu na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake
na ni lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli
mtupu, pia aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa
unapoimba mambo ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa
hujaisaidia jamii husika alisema sugu.
Katika wimbo huo wa 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita yaRuge na Sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera Sugu na kusema
kuwaRoma anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu
umefanya niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu
unanihusu na hakuna ukweli juu ya alichokiimba.
Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili
zimuongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa
jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za
uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss Tanzania ya Solo Thang
atajua anachomaanisha.
Roma alipotafutwa kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma alisema Sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na atamrekebisha.
soucrce:Chumablog
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™