Fikra pekee inayomsumbua Kizito ni jinsi atakavyoweza kumwoa Nusura,
binti mrembo wa mmiliki wa mabanda, Masharubu. Mjomba Mawazo ana wakati
mgumu wa kujadiliana na Masharubu mwenye tamaa ambaye yuko tayari
kumwozesha binti yake kwa mahari kubwa mno.
Cheche bado inamuwia
vigumu kuweka uwiano kati ya biashara yake na familia, na muda wa Cheusi
unapotezwa kwa kuwaangalia watoto wake wawili watundu na mimba yake.
Cheche anapata faraja kwa Tula kwenye Kigrosari chake, huku baadae
studio yake 'ikisambaratishwa' na shangingi linalojiita Lulu linapovamia
toka kusikojulikana na kudai apatiwe huduma!
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™