Blogger Widgets
Home » » WAZIRI WA ULINZI JESHI LA KUJENGA TAIFA AONYA WASANII KUHUSU UVAAJI WA NGUO ZA JESHI

WAZIRI WA ULINZI JESHI LA KUJENGA TAIFA AONYA WASANII KUHUSU UVAAJI WA NGUO ZA JESHI


Katika mkutano wa bunge unaoendelea mjini Dodoma waziri wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha amewaonya wasanii wa Tanzania wanaopenda kuvaa nguo zinazofanana na sare za kijeshi na kudai kuwa kama wakipatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Wapo wasanii ambao wamekuwa wakitumia sare ambazo zinafanana sana na sare za kijeshi narudia tu kwamba ni marufuku kwa watu wasiohusika kuendelea kutumia sare ambazo zinafanana na mavazi ya kijeshi,” alisema Vuai Nahodha.

 

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wasanii wa muziki nchini na hizi ni baadhi ya tweets zao pamoja na wadau wengine.

Mwasiti: wameona wasanii tu…wajadili vya maana uko arrrrgh,siku hizi sitamani hata kucheck bunge wallah,mbona zinatengenezwa na zinaingizwa!?

Nikki Mbishi: Wanajeshi hawaruhusiwi kujihusisha na sanaa nje ya jeshi basi na nyie raia msivuke mipaka yao,sasa bisheni mkione. Watu hawajawahi kupigana vita tangu watoke depo,sasa nyie ligalambueni muone madochi yake mitaani.

Lady JayDee: Sioni kama kuna tatizo lolote. Ni njia ya ku potray kitu tu kwa kukikubali. Mtu aki rap km wewe utachukia? Au utafurahi kuna watu wanapenda kuwa kama wewe?

Young Manilla: so muda wa kukaa na kujadili vitu kama hivyo, na filamu zetu pia zinaitajika ziwe na viwango, sasa picha ya kivita tuvae magunia?

Ms.Hatar ‏: yaaanii ts ridiculous that wana muda wa kujadili hilo suala wakati kuna watoto wanakaa chini darasani smh daaah

Hajeey: ‏waache sanaa ikue na wao ndo wana restrict! Wajidhatiti kwenye mambo ya kuleta maendeleo n stop worrying kuhusu petty things! Vex!!!
source:Bongo5
© Sweetbert Philemon The Lake Zone Link™

0 comments:

Post a Comment

.