Ikiwa bado mixtape yake “Nyota njema ya mtaa” inaendelea
kufanya vizuri sokoni, Chaba a.k.a Baba mkubwa anayewakilisha 009
(Ngalimited)
Arusha city, anawazawadia wapenzi wa muziki wake track mpya na moto
kabisa toka
Grandmaster Records chini ya utayarishaji wa producer John B akiwa
amemshirikisha Jordan aliyetisha na ngoma yake ya mapenzi vita mapema
mwaka huu.
Huyu hapa ni Chaba akiizungumzia track yake mpya;- “Mmmmh!
Hii track basically, ni zawadi kwa mashabiki zangu kwa kuipokea vizuri na
kuinunua mixtape yangu ili pia wasio nazo waendelee kuinunua, na pia bila
kusahau kuwa kawa bado Baba mkubwa nawa-murder rappers wote wanaoigiza sanaa”
Track; Murder
Artists; Chaba feat Jordan
Prod; John B (Grandmaster
Records)
Intro;- Kwa hiyo wee ndio jamaa wanamwita akachaba, Mmmmh! Ni nii
special kuhusu we jamaa haah! Nini special, well mi nilikuja hapa
kuwa-murder!!!!
Verse 1;-
Mistari mara Chaba sawasawa na
mchongo,
Ule ambao ukijumlisha wenye akili
ubongo,
Basi, unapata jumla ya cash
milima, Mgosi wa ndima,
Mama kutoka Meru, Arusha
nimesimama juu kuliko Meru,
Balozi wa Rap kutoka mashariki ya
Africa, Sihitaji malaika,
Kunilinda kitaa, Nipo na mistari
ambayo nikiigawanya haukatiki umeme mitaa,
Una wivu sababu, Mistari yangu
mara doo sawasawa na adhabu,
Kwa yako Career, Wewe ni umbwa
unayelia, Nisipokuwepo nikiwepo unafyata mkia,
Basi, Jifunze kuiheshimu yako
nafasi,
Huu ni urefu wa kamba hufikii kwa
yako kasi, Najumlisha wafuasi,
Nikiwa-murder, Waigiza Hip Hop
nakiwazika bila mashada,
Mi ni crazy Baba, Ndoto
inayokukata stimu ya miaka saba,
Public figure linalochora miraba,
Isiyohesabika kama pundamilia
wote wa Africa na yao
miraba,
Unabakia historia kama Nebukalneza, Huu ni muziki wenye sura haijapendeza,
Kama
mitaa ambayo serikali imeitelekeza,
Rasmi nipo hapa kuwala MC kama supu ya Pweza!
Chorus x 2 Nakubana tuu kwapani, Kwako nastay,
Nakutia shakani, Naku-murder
everyway! Everyway!!
Bridge x 2 Nimechafukwa na roho na hawa mabishoo, Kuja na maswaga
kwa Hip Hop show!! Tunawa-murder,
(Murder)
Verse 2;-
Sikuanza darasa la kwanza kwanza
nilianza, Kuwa MC, Baba mkubwa Macii,
Na nilipogundulika, Kila taa
nyekundu ilibadilika kijani,
Mikono ya maproducer ikaanza
kunyonga kwa wingi majani, Mabiti yakanitamani,
Kila nilipoyarapia yakaniita
Honey,
Zikafa Azonto zikisikia rap
zinazochapa viboko, Kwenye mikoko,
Na kwenye vilabu, MaDJ wakatumia
rap zangu kimatibabu,
Mpaka nikipita mitaa sasa ikawa
balaa, Binti anataka mtoto wangu ili awe staa,
Mi ni jangwa la bahari ya mistari
hadimu,
Na ninanyesha madini masika kila
msimu,
Haizuiliki, Histori haifunikiki,
Tafuteni category kwa hii hamtambuliki,
Chorus x2, Bridge x2, Outro……………………………………{MurdeR!!!!!!!}
© Dvj Sweetp
0 comments:
Post a Comment